Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimkaribisha
Kiongozi wa msafara wa ujumbe kutoka Serikali za Mitaa za China, Makamu
Gavana wa Jimbo la Shandong, Xia Geng kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dares Salaam. Ujumbe huo
umehusisha magavana na wafanyabiashara kutoka nchini China ambapo
ulikutana na Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi. Lengo la mkutano huo ni kudumisha ushirikiano katika
masuala ya biashara na uchumi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia-meza kuu)
akizungumza jambo na Kiongozi wa msafara wa ujumbe kutoka Serikali za
Mitaa za China, Makamu Gavana wa Jimbo la Shandong Xia Geng
(kushoto-meza) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dares Salaam. Wa kwanza kushoto kwa Waziri Nchimbi ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mwamini Malemi, anayefuata ni Mkuu wa Jeshi
la Polisi (IGP) Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Magereza, John Minja.
Ujumbe huo umehusisha magavana na wafanyabiashara kutoka nchini China
ambapo ulikutana na Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Lengo la mkutano huo ni kudumisha ushirikiano
katika masuala ya biashara na uchumi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kulia) akimkabidhi
zawadi Kiongozi wa msafara wa ujumbe kutoka Serikali za Mitaa za China,
Makamu Gavana wa Jimbo la Shandong Xia Geng kwenye Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dares Salaam. Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi.
Viongozi hao walipeana zawadi ikiwa ni ishara ya kuonyesha ushirikiano
kati ya China na Tanzania. Ujumbe huo umehusisha magavana na
wafanyabiashara kutoka nchini China ambapo ulikutana na Waziri Nchimbi
pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Lengo la
mkutano huo ni kudumisha ushirikiano katika masuala ya biashara na
uchumi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani.
No comments:
Post a Comment