Wanakijiji wa kijiji cha Nyamira wameamka na kukuta mwili wa
mwanamke ukiwa umekatwa kichwa na kutelekezwa pamoja na kufungwa mikono
kwa kamba.
Mwili huo ambao unaonyesha kuwa ni wa mwanamke mwenye miaka kati ya
25 hadi 35 amekutwa umevaa jeans pamoja na blouse nyeusi na kutupwa
pembeni ya kijito cha maji mida ya saa 12 na nusu asubuhi.
Wanakijiji hao wamedai kushtushwa na tukio hilo na kusema kwamba ni
kitu cha ajabu kwenye kijiji chao na polisi wa Kenya wametangaza familia
yoyote itakayoona kuna mtu amepotea nyumbani kwao atoe taarifa mapema.
Hii ni video ya ripoti kamili ya NTV ya Kenya
No comments:
Post a Comment