skip to main |
skip to sidebar
TAMKO LA TIMU YA COASTAL UNION KUHUSIANA NA SAKATA LA MCHEZAJI ABDI BANDA
Nimepokea simu nyingi za wapenzi wa Coastal Union pamoja na wanahabari
kutaka kujua kuhusu kijana wetu Abdi Banda kuihama timu yetu.
Tayari
nimeanza kuudhika, kila siku zinazuka habari mpya kuhusu Banda.
Nimezunguza naye amenijibu hajawahi kuzungumza na timu yoyote kuhusu
usajili.
Ni kweli Banda ni mchezaji mzuri, lakini tuna mkataba
naye wa miaka mitatu, utakapoisha atajua kama anataka kuongeza ama
kuhama, lakini si sasa bado tunamuhitaji kuifikisha timu mbali.
Ila kama kuna timu inamuhitaji kwa sasa utaratibu unajulikana, waonane
na viongozi wazungumze na si kumfuata mchezaji kwa mlango wa nyuma ni
kumuharibia kwa wapenzi wake.
Nimeanza kuudhika, leo
nitazungumza na viongozi wa timu pamoja na mwanasheria wetu kuhusu
utaratibu. Halafu nitatoa msimamo wa timu. Ikiwa kuna mwanahabari
anahusika kuihujumu timu ama klabu ya Yanga ni kweli imefanya mazungumzo
na kijana wetu bila kufuata njia sahihi, basi sheria ndiyo
itakayozungumza si Coastal Union.
nimeambatanisha picha mbili zikimuonyesha Banda akisaini mkataba wa miaka mitatu na Wagosi wa Kaya Julai 18 mwaka huu.
HAFIDH KIDO
MSEMAJI COASTAL UNION
25 NOV, 2013
No comments:
Post a Comment