Wakati
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kikiwa kimetangaza kutoa
barua rasmi kwa wanachama watatu wa chama hicho waliovuliwa madaraka
hivi karibuni kwa madai ya kukiuka kanuni na taratibu za chama, mengi
bado yanajitokeza kuhusiana na sakata hilo.
Jijini
Dar es salaam wameibuka wanaojiita viongozi wa Chama hicho kutoka vyuo
vikuu kadhaa nchini na kukitaka chama hicho kumaliza haraka mgogoro huo
kwani utaathiri kupatikana kwa mageuzi ya kweli hapa nchini kwavile
Chadema ndicho chama kinachoaminiwa na vijana wengi hususan wasomi.
Viongozi
hao ni kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam , Likapo Bakari ambaye
amejitambulisha kama katibu wa Chadema chuoni hapo , Jeremia Fumbe
ambaye amejitambulisha kama mwenyekiti wa Chadema tawi la kutoka Chuo
Kikuu cha Ardhi na Nyakarungu Graison ambaye amehitimu chuo kikuu hivi
karibuni.
Wakizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam viongozi hao waliosema
wanawakilisha wenzao wamesema mtikisiko wowote ndani ya chama hicho
utaleta athari na kusababisha vijana wengi kukimbia
Wanachama
wa Chadema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho, Bwana Zito
Kabwe, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk.Kitila Mkumbo na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba
wamevuliwa nyadhifa hizo kutokana madai ya na kupanga mpango wa siri wa
kupindua uongozi wa juu wa chama jambo ambalo Chadema imesema ni kinyume
na Katiba, Maadili na Itifaki ya chama hicho.
Wamepewa
siku 14 kujieleza kwanini wasifukuzwe kwenye chama kutokana na utovu huo
wa nidhamu, huku wenyewe tayari wakiwa wamejibu baadhi ya tuhuma
ikiwemo baadhi kukiri kuandaa waraka huo wa mabadiliko ndani ya chama.
No comments:
Post a Comment