Zanzibar
Heroes imeanza nzuri kampeni yake ya kugombea kombe la GOtv Cecafa
Senior Challenge Cup baada ya kuifunga timu ngumu ya South Sudan 2-1
katika mchezo mgumu wa ufunguzi wa michuano hiyo katika uwanja wa Nyayo
National Stadium Heroes walihitaji dakika 5 tu kupata bao la kuongoza
kupitia Suleiman Kasim. Zanzibar waliongeza bao lao la pili katika
dakika ya 67 wakati mchezaji aliyeingia akitokea benchi Adeyum Saleh
Ahmed alipofunga bao zuri kwa shuti kali lilomshinda golikipa Juma
Jinaro.
Japo
walikuwa nyuma kwa mabao mawili, Sudan waliweza kujikaza na kufunga bao
la kufutia machozi katika dakika ya 75 kupitia mchezaji wao Fabiano
Lako. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Zanzibar waliweza kuondoka
na ushindi ambao umeweza kuwafanya kuongoza kundi lao baada ya wenyeji
Kenya kutoka sare ya bila kufungana na Ethiopia.
No comments:
Post a Comment