Zitto katika Facebook wall yake |
Kuchukua
au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi
(principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana
lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.
Sio posho tu,
hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu,
kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati
huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda
ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011
nilipoacha kupokea posho za vikao.
Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo
tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua
posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo
japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana
maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi
walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu
za afya huko vijijinink.
Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
No comments:
Post a Comment