Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisogeza matofali kwa Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kuyapandisha juu kwa ajili ya ujenzi wa soko la Mulugo Market Mwambani lililopo katika ya kata Mwambani wakati viongozi hao waliposhiriki ujenzi wa soko hilo linalojengwa na Mbunge wa jimbo la Songwe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mh. Philip Mulugo katika kuwakwamua kiuchumi wananchi wa jimbo la Songwe wilayani Chunya, Kinana amemaliza ziara yake katika wilaya hiyo na kesho anaanza ziara katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MKWAJUNI-CHUNYA)
Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Maweni kata ya Mwambani wilayani Chunya kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kulia wakati alipokagua ujenzi wa bweni hilo lililojengwa kwa msaada wa Shirika la maendeleo la watu wa Japan (JAICA) kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi.
Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutokam kwa mkuu wa shule ya sekondari ya Maweni wakati alipokagua ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi ya Saza katika kata ya Saza Mkwajuni Chunya, anayeshuhudia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro.(P.T)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wafugaji katika kijiji cha Mteka kata ya Kapalala.
Wafugaji wa kijiji cha Mteka kata ya Kapalala wilayani Chunya wakimpokea kwa ushujaa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana huku wakiimba nyimbo za kumsifu wakati alipowasili katika kijiji hicho cha wafugaji.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Ndugu Deodatus Kinawiro akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa ajili ya kulnywesha mifugo yao lakini pia kutumia kwa shughuli za kibinadamu kisima hicho kimefungwa mitambo inayovutamaji kwa kutumia upepo Power Wind, kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Mh. Godfrey Zambi.
Kisima chenyewe ndiyo hiki.
wafugaji wakifurahia jambo wakati Kinana alipokuwa akiongea nao.
Abdulrahman Kinana akiuliza jambo wakati akikagua maradi huo katika eneo la matanki ya maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Gegwa Luhende mara baada ya kuzindua mradi huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza na wafugaji kuelekea eneo la kunweshea mifugo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiuliza jambo kutoka kwa injinia wa idara ya maji Wilaya ya Chunya Bw Ndele Mengo wakati akikagua lambo hilo la kunyweshea mifugo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, katikati Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo kulia na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakila chakula kilichoandaliwa na jamii hiyo ya wafugaji kwa ajili ya wageni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kapalala kata ya Kapalala ambalo linajengwa na wakulima wa Tumbaku kupitia taaisis yao ya Chunya Development Trust.
Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo kushoto na mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro kulia wakishiriki kazi ya kusomba tofali katika ujenzi wa bweni la shule ya sekondari ya Kapalala wilayani Chunya,
Mbunge wa jimbo la Songwe Mh. Philip Mulugo akizungumza na wananchi wa Udinde mahali ambapo ndipo alipozaliwa wakati wa mkutano wa hadhara leo.
Wananchi walipanda hata kwenye miti ili kumshuhudia katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Udinde.
Katibu wa CCM wilaya ya Chunya Braison Mwasimba aliyejejea CCM jana akiwapa ukweli wananchi wa kijiji cha Udinde.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubiwa wananchi wa kijiji cha Udinde Mkwajuni leo.
No comments:
Post a Comment