Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 3, 2013

KINANA AWAHUTUBIA WANAMBARALI MJINI RUJEWA


1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya barafu  mjini Rujewa wilayani Mbarali wakati alipofanya ziara ya kikazi akikagua miradi ya maendeleo na kuhamasisha wana CCM ili  kuimarisha uhai wa chama hicho wilayani humo, Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Ruvuma , Mbeya na Njombe akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa Siasa na Uhusiano ya Kimataifa, Katika ziara hiyo Kinana  amepewa taarifa ya ufujaji wa fedha zaidi ya shilingi Bilioni mbili katika halmashauri ya wilaya ya Rujewa .(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUJEWA-MBARALI)2Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi wa Rujewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Barafu mjini Rujewa 3Dr. Asha Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Rujewa mkoani Mbeya.3AMkuu wa mkoa wa Mbeya  Mh Abbas Kadoro akiwahutubia wananchi katika mji hu0 wa Rujewa4Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi akitoa maelezo  kwa Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdularahman Kinana wakati alipotembelea mradi wa Bwawa la kumwagilia  mashanmba wa Mwendamtitu wilayani Mbarali.4AKutoka kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi , Mkuu wa mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana naDr. Asha Rose Migiro wakielekea katika eneo la mkutano.7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman kinana akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya mradi wa umwagiliaji wa Mwendamtitu katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.6Mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali Bw. Adam Mgoyi akisoma taarifa ya ujenzi wa bwawa  la kilimo cha umwagiliaji  la Mwendamatitukatika bonde la usangu wakati Katibu mkuu huyo alipotembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Mwendamtitu wilayani Mbarali, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Mh. Godfrey Zambi na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.8Kinana akiangalia ngoma za utamaduni za kabila la Kimasai

No comments:

Post a Comment