Mabomu ya machozi yakiwa yanapigwa katika mitaa ya Bangkok.
Raia huyu akirusha bomu la machozi kwa askari lililorushwa upande wao
Wapinzani wakijaribu kuvamia ofisi ya waziri mkuu.
Vikosi vya tiba vikiwasaidia waliojeruhiwa katika maandamano.
WAZIRI
Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amekataa madai ya waandamanaji
wanaomtaka ajiuzulu akisema hilo haliwezekani chini ya katiba ya sasa
nchini humo, lakini akasema yuko tayari kwa mazungumzo.
Maandamano
makubwa leo yalifanywa na wananchi ambapo walijaribu kuivamia ofisi ya
waziri mkuu huyo katika mapambano ambayo tangu yaanze watu wane wamekufa
katika machafuko hayo ya kisiasa.
Waandamanaji
wanaoipinga serikali wamemtaka Bi Yingluck kujiuzulu, ambapo mpinzani
wake, Suthep Thaugsuban, amempa siku mbili kufanya hivyo. Waandamanaji
wanataka serikali ichukuliwa na “Baraza la Umma” wakidai serikali ya
Yingluck inaongozwa na kaka yake ambaye aliangushwa, Thaksin Shinawatra.
CHANZO BBC NEWS
No comments:
Post a Comment