Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, December 2, 2013

Kocha amchomoa kikosini Mbuyu Twite



HAKUNA jinsi kiraka wa Yanga, Mbuyu Twite, anaweza kurejea kwenye timu ya Taifa ya Rwanda katika siku za hivi karibuni.
Kocha wa Rwanda, Eric Nshimiyimana, amesema hana mpango na mchezaji huyo baada ya kumwita kwenye mechi dhidi ya Mali akakaidi na kuzima simu.
“Nilimwita kwenye mechi dhidi ya Mali akagoma na simu akazima, hakuna jinsi nchi kubwa kama Rwanda inaweza kumnyenyekea mchezaji mmoja,” alisema kocha huyo aliyeko mjini hapa kwenye mechi za Kombe la Chalenji.
“Ni tabia mbaya kwa mchezaji kuitwa na kukaidi, kocha hawezi kumnyenyekea mchezaji mmoja kwenye timu ya Taifa. Nafasi ya Mbuyu imeshazibwa na vijana wadogo ambao wanafanya kazi kikamilifu. “Hatuwezi kuendelea kuendekeza hizo tabia, tuna wachezaji kama wanne wadogo ambao wanaweza kufanya kazi vizuri kabisa, hakuna haja ya kuangaika na Mbuyu.”
Rwanda iko kwenye kipindi cha mpito cha kusuka kikosi kipya cha wachezaji wengi wa ligi ya ndani kujiandaa na michuano ya Afrika miaka ijayo.CHANZO MWANASPOTI


No comments:

Post a Comment