skip to main |
skip to sidebar
Kocha wa Simba "Kibadeni" aporwa gari...
Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni.
Na Wilbert Molandi
ALIYEKUWA
Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni, amenyang’anywa gari aina ya
Toyota Mark 11 GX 110 alilopewa na uongozi wa timu hiyo akiwa anakinoa
kikosi hicho.
Kocha huyo hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo yeye
na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kabla ya yeye mwenyewe
kutangaza kujiuzulu kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Tetesi zilizopo hivi sasa ni kwamba, gari hilo anatarajiwa kupewa
kocha mpya wa timu hiyo, Zdravok Logarusic, raia wa Croatia, aliyetua
jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Kocha huyo anatarajiwa kukabidhi gari wakati wowote kuanzia hivi
sasa, mara baada ya kukamilisha baadhi ya vitu, ikiwemo kusaini mkataba
wa kuifundisha timu hiyo.
Uongozi huo utampa kocha huyo gari hilo kwa ajili ya matumizi ya timu na binafsi katika mizunguko yake mbalimbali nchini.
Gari
hilo analotarajiwa kupewa, awali lilikuwa likitumiwa na aliyekuwa kocha
mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, raia wa Serbia, kabla
hajatimuliwa.
Alipotafutwa Kibadeni kuzungumzia hilo, alisema:
“Nimeshakabidhi kila kitu kwa Simba, sitaki kuzungumza masuala yoyote ya
timu hiyo kwa sasa.”CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment