Pages

Tuesday, December 10, 2013

Maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa


………………………………………………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
NCHI za Afrika zimetakiwa kujenga umoja na kupeana uzoefu katika vita
vya kupambana na rushwa huku  nchi hizo zikitakiwa kujenga sera za uwazi kwenye sekta nzima ya rasilimali ili waweze kunufaika nazo ikiwa
ni pamoja na kupaza sauti moja kuomba kurejeshwa kwa fedha zilizoko nje ya bara la Afrika.
Hayo yalielezwa jana na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia
Utawala Bora Mh.George Mkuchika alipokuwa akifunga na kusherehekea
maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa pia maadhimisho ya miaka kumi ya mkataba wa umoja wa Afrika yaliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa elimu ina nguvu katika kupambana na rushwa hivyo ili kuhakikisha kuwa swala hilo linatokomezwa na nchi za Afrika zinapaswa kutekeleza kwa vitendo mkataba wa umoja wa Afrika dhidi ya rushwa kwa kila nchi kujiunga moja kwa moja kwa kutoa uzoefu juu ya mapambano dhidi ya rushwa ambayo yameonekana kurudisha nyuma maendeleo ya bara la Afrika.
Alieleza kuwa pamoja na chi za Ulaya kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya rushwa lakini nchi hizo zimekuwa zikikumbatia wahamishaji wa fedha kutoka bara la Afrika na kukaa kimya kila wanapotakiwa kurejesha fedha zilizopo kwenye mataifa hayo.
“Mnakumbuka kwa kipindi cha nyuma wapo baadhi ya viongozi waliokamatwa kwa kulimbikiza fedha katika mabenki ya nchi za nje ya bara la Afrika hadi sasa fedha hizo bado hazijarejeshwa na mataifa hayo na mataifa hayo kushikwa na kigugumizi licha ya kuhubiri vita dhidi ya rushwa hivyo ni vema mataifa yetu ya bara la Afrika yakaungana kupaza sauti ili fedha hizo zirejeshwe ili zisaide maendeleo ya bara la afrika”aliongeza Mkuchika.
Aidha alifafanua kuwa nchi 30  zimesaini mkataba wa umoja wa mataifa wa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 44 zinazotakiwa kusaini mkataba huo hivyo kuzitaka nchi zilizobaki kujiunga na umoja huo ili kuliletea maendeleo bara la Afrika na kuwa na sauti moja ya mapambano dhidi ya rushwa huku akizitaka nchi za bara la afrika kutambua kuwa mapambano ya rushwa si ya mtu moja bali ya watu wote.
Nae Mkurugenzi wa takukuru nchini Dr. Edward Hosea alisema kuwa bara la Afrika bado lina safari ndefu katika mapambano ya vita vya rushwa kwani kati ya nchi za afrika 34 kati ya 44 ndizo amabazo zimesaini mkataba wa mapambano ya rushwa huku akidai kuwa mikataba mingi inaingia kwenye rasilimali za nchi za bara la Afrika haina uwazi na sheria zinazotumika  hazimnufaishi mwananchi wa kawaida dhidi ya mapambano ya rushwa.
Aidha Hosea aliitaka serikali kuweka sera ya uwazi kwenye mikataba ya wawekezaji wa rasilimali ya gesi ili iweze kuwanufaisha watanzania na sheria zitakazotungwa iwe ya uwazi na yenye faida kwa watanzania huku akizishawishi nchi ambazo hazijatakeleza mkataba wa umoja wa mataifa zifanye hivyo mara moja kwani bara la Afrika ndilo linalohitaji maendeleo makubwa hivyo bila kuungana hawataweza kufanikiwa.

No comments:

Post a Comment