Mjombaake Rais Barack Obama wa Amerika, Bw Onyango 'Omar’ Obama/ Photo via bostonglobe
Mjomba wa
Rais Barack Obama wa Amerika, Bw Onyango 'Omar’ Obama, ameruhusiwa
aendelee kuishi nchini humo na Mahakama ya Uhamiaji kwenye uamuzi kuhusu
kesi ya kufukuzwa kwake uliotolewa Jumanne.
MJOMBA wa
Rais Barack Obama wa Amerika, Bw Onyango 'Omar’ Obama, ameruhusiwa
aendelee kuishi nchini humo na Mahakama ya Uhamiaji kufuatia kesi ya
kufukuzwa kwake iliyofanyika Jumanne.
Jaji wa
Uhamiaji Amerika, Bw Leonard Shapiro alimruhusu Bw Onyango mwenye umri
wa miaka 69 aendelee kuishi nchini humo na kumzuia kuhamsishwa Kenya,
kwa kusema ametimiza mahitaji ya kukabidhiwa kibali cha 'Green Card’.
Kwenye uamuzi wake, Jaji huyo alisema anaamini Bw Onyango ni muungwana, jirani mwema na hulipa ushuru inavyohitajika.
Jaji
Shapiro alisema anatumia sheria inayoruhusu wahamiaji wasiotambulika na
taifa lolote wawe wakazi wa kudumu ikiwa waliwasili Amerika kabla 1972,
wakaendelea kuishi huko na wenye tabia njema.
Bw Onyango amekuwa akiishi Amerika kwa miaka 50 sasa, kwani aliwasili huko 1963.
Alikuwa ameamrisha kuhama 1992 ingawa alikaidi agizo hilo na akabaki nchini humo.
Haikujulikana alikuwa bado yuo Amerika hadi alipokamatwa kwa kuendesha gari akiwa
mlevi 2011, mjini Framingham, magharibi mwa Boston.
Baada ya kukamatwa kwake, amri ya kuhamishwa kwake iliyokuwa imetolewa awali ilianza kujadiliwa upya.
Alifikishwa
mahakamani alipokamawa akiendesha gari akiwa mlevi ingawa Jaji
aliyesimamia kesi hiyo aliiendeleza kwa mwaka mmoja bila kutoa hukumu,
na kusema kesi hiyo ingeondolewa iwapo Bw Onyango hatakamatwa tena
wakati huo.
Alipoulizwa na Mahakama ya Uhamiaji ikiwa alikuwa na familia Amerika, alisema, “Nina mpwa. Barack Obama, ndiye Rais wa Amerika.”
Bw
Onyango sasa ameruhusiwa kuomba kuwa mkazi wa kudumu, ambayo itampatia
haki ya kufanya kazi kihalali Amerika na kusafiri nje ya nchi hiyo.
Mnamo Mei
2010, dadake Zeituni Onyango aliruhusiwa kuishi Amerika baada ya kudai
kwa kuwa ni Mjaluo, maisha yake yangekuwa hatarini iwapo angehamishwa
kurudi Kenya.
Bi Onyango aliwasili Amerika 2000, na alijaribu kuomba aruhusiwe kuishi Amerika 2004 ingawa aliamrishwa kuhama na Jaji Shapiro.
Hata
hivyo, Bi Onyango hakuhama na badala yake aliishi katika nyumba
zinazomilikiwa na Serikali ambazo kwa kawaida hutumiwa na wakazi halali
wa Amerika na wananchi wenye mapato ya chini, ambao huwa hawaitajiki
kuzilipia au hulipa kiasi kidogo cha pesa.
Punde
baada ya ombi lake la pili kuruhusiwa, alinukuliwa kwenye vyombo vya
habari akisema Amerika ilikuwa na haki ya kumruhusu awe raia kwa kuwa
alikuwa mhamiaji.
“Ikiwa nilikuja kama mhamiaji, mko na jukumu la kunifanya niwe raia,” aliambia kituo cha televisheni cha WBZ kilicho Boston.
Ingawa
Zeituni Onyango na kakake wanaweza kuishi Amerika kihalali na kusafiri
nje ya nchi wanavyotaka, Bi Onyango hawezi kusafiri kuelekea Kenya kwa
kuwa alikabidhiwa uraia kwa misingi ya kuwa ilikuwa hatari kwake kuwepo
Kenya.
Chanzo: swahilihub.com
No comments:
Post a Comment