Akizungumzia tukio hilo meneja wa mamlaka ya mapato
mkoani Kagera Bw. Leonard Shija pamoja na kueleza uimara wa kikosi
chake cha doria amesema mkoa huo wenye vituo nane vya kuvukia kwenda
nchi tatu za uganda, rwanda na burundi umekuwa na changamoto ya njia
nyingi pamoja njia ya maji kupitia ziwa victoria na hivyo kuihitaji
msaada wa taasisi zingine pamoja jamii kwa kutoa taarifa kwa manufaa ya
nchi na watu wake.
Hata hivyo afisa forodha Bw. Mayela Baluhi na
mwelimishaji elimu kwa umma TRA mkoani Kagera Bw. Lutufyo Mtafya
wamesema operesheni hiyo walioielezea kuwa ya kudumu katika udhibiti wa
magendo mkoani humo wamesema imefanikiwa kudhibiti uiungizaji bidhaa
holela na ukwepaji kodi wakati wa kuvusha katika vituo vya Mtukula,
Mulongo, Rusumo, Kabanga,Murusagamba na Kanyigo huku njia za panya
zikibakia kuwa changamoto kubwa inayohitaji elimu ya uzalendo wa
kudhibiti magendo nchini.
Naye mkaguzi wa chakula na kaimu meneja wa mamlaka
ya chakula na dawa nchini TFDA kanda ya ziwa Bi. Nuru Mwasulama pamoja
na kueleza viroba hivyo aina ya Raider, Empire na Signature kutokuwa na
vibari vya kuingizwa nchini amesistiza kuwa na uwezekano wa kuathiri
afya za binadamu moja kwa moja au kwa muda mrefu huku akieleza jitihada
za mamlaka hiyo katika udhibiti wake kuanzia mipakani na ndani ya ukanda
huo ambao umeonekana kuwa soko lake kuu.chanzo ITV
No comments:
Post a Comment