Hayo yamesemwa na waziri wa ujenzi Dakt John
Magufuli wakati wa utiaji saini mikataba ya kutengeneza barabara
itakayounganisha kipande cha kutoka Capetown hadi Kairo kilichokuwa
kimebakia kwa upande wa Tanzania itakayopitia mikoa ya Dodoma na Manyara
ambapo amewatahadharisha wakandarasi hao kutosaini mikataba hiyo kama
hawana uhakika wa uwezo wao wa kujenga barabara hizo kwa muda
uliopangwa.
Aidha Dkt Magufulu ameongeza kuwa serikali
haitayavumilia magari yote yatakayozidisha uzito kwa kisingizia chochote
kwani barabara hizo zinatengenezwa kwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo
nyingi ni za walipa kodi pamoja na mikopo kutoka sehemu mbalimbali.
Awali mtendaji mkuu wa Tanroads mhandisi Patrick
Mfugare amesema wametumia taratibu zote katika kuwapata wakandarasi
watakaochukua miradi hiyo kwa lengo la kuepuka wakandarasi wasiokuwa na
uwezo ambao wengi wamekuwa wakiiletea serikali hasara sambamba na
kuchelewesha kukamilika kwa miradi husika.
Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa na baadhi ya
wabunge wa maeneo yote ambayo ujenzi huo utapitia ambao mbali na
kuelezea kufurahishwa na hatua hiyo wamesema barabara hizo zikimalizika
zitasaidia sana hasa kwa upande wa biashara sambamba na kupunguza
gharama za usafirishaji.chanzoITV
No comments:
Post a Comment