Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 29, 2014

ALHAJI KUNDYA KUMNADI MAHMOUD THABIT KOMBO LEO CCM MBWENI

 Mahmoud akiwa na binti yake wakati wa kampeni zilizofanyika jana uwanja wa Bustanini.
 Mgeni rasmi wa leo Alhaj Mwangi Kundya
Na Andrew Chale, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi CCM, leo Januari 29, kinatarajia kufanya kampeni yake ya Saba  (7) ya mkutano wa hadhara kwenye eneo la uwanja wa tawi la CCM, Mbweni, Kiembesamaki, katika kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki,  ambapo mgeni rasmi wa kumnadi Mgombea anatarajiwa kuwa, Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini, Alhaj Mwangi Kundya.

Akielezea mkutano huo wa Saba, mapema leo, unaotarajiwa kuwa majira ya Saa kumi jioni, eneo hilo la CCM Mbweni, Mahmod Thabit Kombo ,  aliwaomba wananchi wa wa Kiembesamaki kufika kwa wingi kwenye mkutano huo, ambapo pia kutakuwa na shamrashamra mbalimbali zitakazoanza majira ya Saa Nane, mchana. Hivyo amewaomba wananchi  kujitokeza kwa wingi ilikumsikiliza na kuzijua sera za Chama katika kuwaletea maendeleo.

“Leo Januari 29, nawaomba  wananchi wa Kiembesamaki, kujitokeza  kwa wingi eneo la CCM Mbweni, ilikusikiza sera , Ilani na mipango endelevu tuliyojipangia ndani ya chama” alisema Mahmoud Thabit Kombo.

Aidha, aliwaomba wananchi wa Jimbo hilo,  ifikapo Februari 2, 2014 siku ya Jumapili, kumpa kura za NDIYO, ili awe Mwakilishi wao atakayeenda kuwatetea Bungeni  kwenye Baraza la Wawakilishi, sambamba na kumaliza kero zinazowakabiri.

Baadhi ya mambo, mbalimbali anatarajia kuzungumzia siku ya leo kwenye mkutano huo ikiwemo kero za maji, elimu, kuwezesha vijana, akinamama na jamii nzima ya jimbo hilo la Kiembesamaki, pindi watakapomchagua kuwa mwakilishi wao

No comments:

Post a Comment