Pages

Tuesday, January 7, 2014

ASKARI POLISI AJIPIGA RISASI MKOANI SHINYANGA.


 
PC David Alfred
Akizungumza na waandishi wa habari  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala amesema tukio la askari wake aitwaye David Alfred (25-30)kujeruhiwa kwa risasi limetokea jana majira ya sa 12 na nusu jioni wakati askari huyo akikagua silaha aina ya SMG katika ghala la silaha katika kambi ya jeshi la polisi mjini Shinyanga ili aingie kazini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kuhusu tukio la askari kujeruhiwa kwa risasi 

Amesema wakati askari huyo akikagua silaha hiyo ghafla risasi ilifyatuka na kumjeruhi chini ya bega la mkono wa kushoto hali iliyopelekea akimbizwe katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

Amesema tukio hilo ni bahati mbaya tu huku akiwataka askari polisi kuwa makini na kujali usalama wao kwanza kabla na wakiwa kazini.
Dkt Fredrick Mlekwa akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mkoa Shinyanga Dkt Fredrick Mlekwa amesema hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri anaongea, vizuri na kwamba kufuatia tukio hilo askari huyo amepata majeraha katika sehemu za kifuani na mkono wa Kushoto.

No comments:

Post a Comment