Pages

Wednesday, January 22, 2014

HAWA NDO WATU WALIOKAMATWA KWA SHAMBULIO LA WASTEGATE NCHINI KENYA


2 
Ripota wangu wa nguvu Julius Chemitei kutoka Nairobi anaripoti kwamba Hakimu na pande husika dhidi ya washukiwa wa shambulio la Westgate wametembelea eneo la tukio kutekeleza amri iliyotolewa na hakimu mkuu Daniel Ojenja wiki iliyopita kabla ya kesi hiyo kuahirishwa.
Hakimu Daniel Ochenje alizungumza na waandishi kwenye hii ziara na kusema umuhimu wa ziara hiyo ni kuwezesha pande husika kupata taswira ya eneo hilo wakati Mashahidi wanapolihusisha eneo la tukio kwenye ushahidi wao Mahakamani.
Mawakili wa washukiwa wanaendelea kusimamia kwamba wateja wao hawana hatia yoyote na baada ya ziara hiyo walikua tayari kuendelea na kushirikiana na Mahakama wakati wakisubiri uamuzi kutolewa.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tarehe 27 & 28 January 2014 wakati upande wa mashtaka ukitarajiwa kuwasilisha mashahidi wengine 28 ambapo hata hivyo kumekuwa na malalamiko kutoka kwa mawakili wa upande wa Washukiwa kwamba viongozi wa mashtaka hawajawapa taarifa za polisi zilizoandikishwa na mashahidi.
3
1
6 
Hawa ni baadhi wa washukiwa wenyewe wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la Westgate.
5
4

No comments:

Post a Comment