Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 22, 2014

JK APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI WA OMAN NCHINI

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Oman hapa nchini Mhe.Soud Ali Bin Mohamed Al Ruqaishi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2014.

Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Ruqaishi Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Ruqaishi, Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Ruqaishi (wa pili kushoto) na Maafisa waliofuatana na Balozi huyo.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi Ruqaishi mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Balozi Ruqaishi akimshukuru Kiongozi wa Bendi ya Polisi. Picha na Rosemary Malale, Mambo ya Nje

No comments:

Post a Comment