Mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote akiendesha Ibada ya mazishi. |
Kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole |
Marehemu Gabriel Osward Ngalele. enzi za uhai wake |
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of God[TAG]Uyole akiongea na mwandishi wetu ambae hayupo pichani |
Katikati mke wa Marehemu |
Mwili wa marehemu ukiagwa makaburini hapo |
Na Ezekia Kamanga - Mbeya Yetu
Mchungaji Edward Mtweve wa kanisa la Tanzania Assemblies of
God[TAG]Uyole Njia Panda amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya
Waendesha pikipiki[Bodaboda]kuvuruga ibada ya mazishi ya mwendesha
pikipiki aitwaye Gabriel Osward Ngalele.
Vurugu hizo zilitokea katika Kanisa hilo baada ya Gabriel Ngalele
kufariki kwa ajali ya gari Januari 13 majira ya saa 11 alfajiri eneo la
SAE akiwa na abiria wake ambapo walifariki papo hapo baada ya kugongwa
na Roli.
Taratibu za mazishi zilipokamilika mwili wa marehemu ulipelekwa katika
Kanisa hilo wakati mchungaji akiendesha Ibada aliomba utulivu kwa wafiwa
ambapo walitulia lakini vijana zaidi ya 300 waendesha bodaboda
walilipuka kwa kelele hali ilyomfanya mchungaji kuomba utulivu katika
Ibada.
Hata hivyo vijana hao waliendelea kujaa katika kanisa hilo na kukosekana
utulivu hali iliyomlazimu mchungaji kuwaambia kama wamekosa utulivu
basi watakuwa wamefuata ubwabwa katika msiba huo hali iliyofanya kutokea
mtafaruku mkubwa.
Katika mtafaruku huo ilpelekea vijana kuuchukua mwili wa marehemu hadi
kwenye makaburi huku wakimwacha mchungaji ambapo ililazimu jeshi la
polisi kuingilia kati na kuzuia fujo kanisani na kuamua kumresha
nyumbani kwake kwa ulinzi mkali.
Wakati mchungaji akisindikizwa nyumbani kwake vijana waliendelea na
taratibu za mazishi kwa utaratibu uliosimamiwa na Mwenyekiti wa Bodaboda
Jiji Vicent Mwashoma huku mchungaji wa Bodaboda Bahati Mwasote
akiendesha Ibada ya mazishi.
Katika mazishi hayo baadhi ya Viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo
mlezi wao Nwaka Mwakisu,Mlezi wa Bodaboda Taifa Respisius Timanywa
ambaye aliwaasa vijana kuhudhuria mafunzo ili kupunguza ajali za mara
kwa mara.
Kwa upande wake mchungaji Edward Mtweve wa Kanisa la TAG amesema
amesikitishwa sana na kitendo cha kuvurugwa kwa Ibada kwani amesema kuwa
wengi wa waliokuwa wakifanya fujo walikuwa ni walevi na wavuta bangi na
si waumini wa Kanisa lake.
Aidha Mtweve na Baraza la wazee wamesema kuwa hawakusudii kuchukua hatua
zozote dhidi ya vijana ambao wamefanya fujo kwani yote wanamwachia
Mungu na kwamba katika kanisa hilo hakuna tukio lilowahi kutukia.
Pia amesema kitendo cha kuchukua mwili wa marehemu madhabahuni ni cha
utovu wa nidhamu kwani vijana wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu.
Wakikabidhi rambirambi kwa mjane ,Mwenyekiti wa Bodaboda Jiji Vicent
Mwashoma amesema pesa za rambirambi zitumike kusaidia familia ya
marehemu badala ya ndugu kutumia pesa hizo kuendeshea msiba huo.
No comments:
Post a Comment