Pages

Sunday, January 12, 2014

KAMPUNI YA VIJANA WA KITANZANIA YA (China Word Buz) KUWAKOMBOA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI

1Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz na mwakilishi wa wamiliki wa viwanda 45 nchini China vilivyoingia mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo China Bwana Cheng Wang Wu kushoto akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere huku akiwa ameongozana na Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wakilakiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande, kampuni hiyo imeanzishwa nchini ikiwa na lengo la kuwakomboa na kuwasaidia wafanya biashara wadogo na wa kati nchini Tanzania ili kutafuta masoko na kuwapa taarifa sahihi za masoko na biashara nchini China ambapo wanatarajia kuendesha semina kwa wafanya biashara  katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. 2Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kwasili akitokea nchini China na ujumbe wa wafanya biashara wenzake, kushoto ni Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu na kulia ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande 3Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo hapa nchini Bw. Shafii Mwaijande wa pili kutoka kulia ,Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda wa tatu kutoka kulia na Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya  China Word Buz nchini China Bwana Cheng Wang Wu wa tatu kutoka kushoto wakiwa na wafanya biashara wenzao. 4Meneja Mkuu  wa kampuni hiyo nchini China Justin Luvanda akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.

No comments:

Post a Comment