Pages

Friday, January 24, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AANDAA SHERRY PARTY KWA WAKE WA MABALOZI WA NCHI ZA NJE WAISHIO HAPA TANZANIA.




Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya (sherry party) aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa nchini. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.1.2014.
Kiongozi wa Umoja wa wake wa mabalozi waliopo hapa Tanzania Mama Celine Mpango, (ambaye ni Mke wa Balozi Juma Mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) akitoa salamu zake kwa niaba ya wanajumuia hiyo wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Ikulu Trahe 23.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mume wa Balozi wa Zambia hapa nchini Bwana Victor Nsemiwe wakati wa sherry party aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko hapa Tanzania. Sherehe hiyo ilifanyika Ikulu tarehe 23.01.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wake wa mabalozi wa nchi za nje walioko Tanzania pamoja na wageni wengine huko Ikulu tarehe 23.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mke wa Balozi wa DR Congo Mama Celine Mpango (kushoto), Mama Asha Bilal (mke wa Makamu wa Rais), Mama Sitti Mwinyi na mwisho ni Mama Anna Mkapa wakielekea sehemu ya tafrija mara baada ya kupiga picha ya pamoja.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mama Celine Mpango (kushoto) akifuatiwa na Mama Sitti Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi, Mama Asha Bilal na Mama Anna Mkapa.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mama Celine Mpango na Mama Asha Bilal wakati wa sherry party aliyowaandalia wake wa mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania huko Ikulu tarehe 23.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

Post a Comment