skip to main |
skip to sidebar
MAPINDUZI CUP:::SIMBA WAVUTWA SHATI NA KCC KWA SARE TASA
Wekundu wa Msimbazi Simba wameshindwa
kuwatambia KCC ya Uganda baada ya kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya
bila kufungana katika mchezo wa kundi B kuwania Kombe la Mapinduzi
uliochezwa uwanja wa Amaan usiku huu.
Kwa ujumla timu zote
ziulionekana kucheza kwa umakini mkubwa hasa katika safu za ulinzi ikiwa
ni ishara ya kuepuka kupoteza mchezo na kubakiza matumaini ya kufuzu
kwa robo fainali. ambapo hadi mapumziko timu zote zilikuwa zimepiga
mikwaju miwili tu iliyolenga lango la mpinzani.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Kipindi cha pili Simba ilionekana kuimarika zaidi hasa baada ya kuingia
kwa Said Ndemla kuchukua nafasi ya Amri Kiemba na pia Betram Mwombeki
aliyechukua nafasi ya Amissi Tambwe, ambaye alionekana kukosa ujanja wa
kuipenya ngome ya waganda kwa kudhibiwa vilivyo. Kwa ujumla Simba
walipiga mikwaju mingi zaidi iliyolenga lango kwani walipata mikwaju 6
wakati KCC walipiga mitatu
Simba Nusura waandike bao katika mwa
kipindi chapili pale Ndemla alipopiga mkwaju mkali ambao hata hivyo
uliokolewa na mlinda lango na ukawa kona butu.
KCC wangeweza
kuandika goli la kusawazisha katika dakika za mwisho kabisa za mchezo
kamasi uhodari wa mlinda lango Ivo Mapunda kuuucheza mpira uliokuwa
ukielekea langoni na kufanya timu zote mbili zifune alama moja na
kufikisha alama nne.
KCC iko kilelelni mwa kundi B ikiipiku
Simba kwa wingi wa magoli ya kufunga wakati AFC na KMKM zinashika nafasi
ya tatau na ya nne kwani zote zina alama moja kila moja. Michezo ya
mwisho keshokutwa ndiyo itaamua ni tiu ipi iende robo fainali wakati
Simba itakapocheza na KMKM na na KCC wakiikabili AFC Leopards
Kesho Jumamosi kuna michezo mine. Kwenye uwanja wa Gombani Pemba watoza
ushuru wa Uganda, URA watapepetana na timu mseto ya Pemba (Clove Stars)
kuanzia saa 8 mchana na baadaye saa 10 Mbeya CITY watakipiga na timu ya
Chuoni.
Wakati hayo yakiwa Pemba, Unguja kwenye uwanja wa Amaan
saa 10 jioni Ashanti United wataonyeshana kazi na timu mseto ya unguja
(Spice Stars) na sa 2 usiku mabingwa watetezi Azam watawakabili Tusker
ya Kenya.
No comments:
Post a Comment