Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 23, 2014

MESSI AWA MPISHI BARCA IKIITANDIKA 4-1 LEVANTE

article-2544195-1AE34E5600000578-624 634x4351 44d91
TIMU ya Barcelona imemaliza hasira zake za sare ya Jumapili na Levante kwa kuifumua timu hiyo mabao 4-1 usiku huu kwenye Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Uwanja wa Ciutat de Valencia. (HM)
Mkali wa mabao wa Barca, Lionel Messi amecheza mechi ya 400 katika timu hiyo Katalunya usiku huu, ambazo ndani yake ameshinda mataji sita ya La Liga na matatu ya Ligi ya Mabingwa.

Messi alifanya kazi nzuri akitoa mchango kwa mabao yote manne, ikiwemo hat-trick ya Cristian Tello. Wenyeji walitangulia kupata bao lililofungwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool, Nabil El Zhar.

Juanfran alijibabatiza mpira uliopigwa na Messi na akaudondoshea kwenye nyavu zake mwenyewe kuisawazishia Barca- kabla ya Tello kufunga mara tatu mfululizo kuipa ushindi mtamu timu yake. Chanzo: binzubeiry
 TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment