WAKATI
sehemu ya makaburi imekuwa ikiogopwa na watu wengi kutokana na ukweli
kwamba ni makazi ya wafu, hali ni tofauti kwa mtoto wa kiume
anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 8-9 ambaye jina lake
halikuweza kufahamika, kuishi katika makaburi ya Kigilagila, Yombo
jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya mwezi mmoja. Taarifa
zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadaye kufuatiliwa kwa karibu na
waandishi wetu, zinasema mtoto huyo ambaye hafahamiki alikotokea,
alionekana akishinda na kulala katika makaburi hayo kwa zaidi ya mwezi
mzima uliopita, kabla ya kutoweka kuelekea sehemu isiyojulikana.
Lakini
baada ya siku kadhaa za kutoweka kwake, majirani wanasema walimuona
tena mtoto huyo akiendelea na maisha eneo hilo ndipo walitoa taarifa
Kituo Kidogo cha Polisi Yombo kuwataarifu juu ya tukio hilo lisilo la
kawaida.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)
Polisi
walifika makaburini hapo na kumchukuwa kijana huyo lakini walipomuhoji
hakuweza kuongea chochote, hali iliyowafanya askari hao kutojua cha
kufanya.
Kutokana
na hali hiyo, polisi wa Kigilagila walifanya mawasiliano na Kituo cha
Buguruni kwa hatua zaidi, ikiwemo kubaini anakotoka na sababu za kuishi
katika mazingira hayo.
Gazeti
hili lilifika na kumkuta mtoto huyo akiwa katika Kituo cha Buguruni
anakohifadhiwa wakati ndugu au wazazi wakisubiriwa, kabla ya taratibu
za kumkabidhi kwa Ustawi wa Jamii kuanza kuchukuliwa.
Aidha,
vyanzo vyetu ndani ya kituo hicho vilisema kuna watu walijitokeza
wakiwa wanatafuta mtoto wa namna hiyo, lakini baada ya kumuona, walisema
hakuwa yeye.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi alithibitisha
kuwepo kwa mtoto huyo na kwamba taratibu zinafanywa ili kulimaliza
tatizo lake.
“Natoa
wito kwa wananchi waliopotelewa na kijana mwenye umri huo, kufika
katika Kituo cha Polisi Buguruni ili kuweza kumtambua mtoto huyo,”
alisema Kamanda Minangi
No comments:
Post a Comment