Pages

Tuesday, January 28, 2014

MUME AMNYONGA MKE NA KUMTUMBUKIZA CHOO CHA KANISA


Watu watatu wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio matatu tofauti likiwemo la John Kaguo (30) mkazi wa Usokami kumuua mkewe bi Jane Makombe (25) mkazi wa Lutuna kwa kumnyonga shingoni na kisha kumtumbukiza kwenye choo cha kanisa.
  Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 25 januari usiku huko maeneo ya kijiji cha Ihalimba kata ya Ihalimba tarafa ya Kibengu wilaya ya Mufindi.
Mungi alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa mahojiano Zaidi huku chanzo cha tukio hilo la kinyama likichunguzwa.
Na katika tukio lingine bi Neema Luwumba (33) mkazi wa Lugalo alifariki dunia katika Hospitali ya mkoa alipokuwa akiendelea na matibabu baada ya kupigwa na shoti ya umeme maeneo ya Mkimbizi.
Kamanda Mungi alisema marehemu alikutwa na janga hilo la kupigwa na shoti alipokuwa akianika nguo alizokwisha kuzifua katika kamba inayosadikika kuwa ni waya wa umeme.
Mbali na matukio hayo mawili, Kamanda Mungi alisema mwanaume mmoja jina Juma Cheles (60) alifariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na pikipiki  huko maeneo ya kijiji cha Nzivu Mafinga wilaya ya Mufindi.
Marehemu alikuwa akiendesha pikipiki aina ya sunlg yenye namba za usajili T 609 BHJ aligongana na pikipiki yenye namba za usajili T 268 BZR Sunlg mali ya Benedict Mwanjombe (30) na kufariki papo hapo, huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa ni mwendo kasi.
chanzo
www.matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment