Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 30, 2014

MWIGULU NCHEMBA ATUA IRINGA,AWASHA MOTO WA KAMPENI UCHAGUZI WA MADIWANI

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba hii leo ameingia Mkoa wa Iringa kwaajili ya Kufanya Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani unaoendelea Nchini.Picha ni Mh;Mwigulu Nchemba akihutubia mamia ya Wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM kitongoji cha Mawambala Kata ya Ukumbi Wilayani Kilolo mapema hii leo tar.29.01.2014.Ki historia Kata ya Ukumbi haijawahi kutawaliwa na Upinzani,na Jimbo la Kilolo linaongozwa na CCM kwa nyanja zote za Udiwani,na serikali za Mitaa zote.

 Mh;Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara viwanja vya CCM kata ya Ukumbi.
Naibu Katibu Mkuu akimnadi Mgombea wa Udiwani kwa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Gift Emmanuel hii leo Kata ya Ukumbi wakati wa Mkutano wa hadhara wa kunadi sera za Chama Cha Mapinduzi kwa Wananchi.
 Naibu Katibu Mkuu CCM Mh;Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha(sera) akisisitiza Kuwa CCM imeiongoza Kata ya Ukumbi tangu miaka 37 iliyopita,Kunamaandeleo mengi yamefanyika ikiwamo Ujenzi wa Barabara,Zahanati,Mashule na Pembejeo za Kilimo,Na kwakuwa Diwani aliyefariki alikuwa wa Chama Cha Mapinduzi,hivyo Wanaukumbi wahakikishe wanampata Diwani mwingine wa CCM iliaendeleze utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye kata hiyo.Ni rahisi sana kutimiza ilani yote kwa Wanaukumbi endapo mtamchagua Diwani wa CCM kwa sababu CCM ndio Chama kinachounda Dola pia ndicho Chama kinachotekeleza ilani kwa sasa,Kuchagua Upinzani ni sawa na kujizibia maendeleo kwa sababu Upinzani hawana Ilani yoyote ya Kutekeleza kwa Kata yenu,Vilevile huu sio Uchaguzi Mkuu kwamba Diwani atabadilisha Serikali,Serikali iliyopo madarakani niya CCM na Shughuli zote za maendeleo zinasimamiwa na CCM,Hao wengine ni wapinzani wa kila kitu na mkiwakaribisha hapa watakuja kuwaletea Vurugu mpoteze amani mliokuwa nayo Tangu uhuru.
 Mh;Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama Cha mapinduzi kitongoji cha Mawambala,Kata ya Ukumbi Mkoani Iringa.Amewaomba Tar.09.02.2014 Wanachi wote kujitokeza Kupiga kura kwa wingi kuichagua CCM iendelee kuongoza kata ya Ikumbi chini ya Diwani Gift Emmanuel.

Picha zote na Habari Kwanza Blog

No comments:

Post a Comment