Pages

Sunday, January 12, 2014

NAIBU KATIBU MKUU MHE. MWIGULU NCHEMBA AHANI MSIBA WA MAREHEMU ZAINAB BUZOHERA.


Naibu Katibu Mkuu CCM Mh:Mwigulu Nchemba akitoa pole kwa Baba Mzazi wa Marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Nchini Marekani wiki iliyopita. Wakati wa Uhai wake Marehemu alikuwa Kada mtiifu wa Chama cha Mapinduzi  na alifariki siku ya Jumamosi Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community iliyopo Lanham, Maryland nchini Marekani.

Mh. Mwigulu Nchemba akisalimiana na mmoja wa viongozi wa Kidini waliofika Msibani hapo Ukonga(babana) Jijini Dsm.
Mh. Mwigulu Nchemba Mbunge wa Iramba Magharibi akisalimiana na Kutoa Pole kwa Mama Mkwe wa Marehemu Zainab Buzohera hii leo alipowatembelea Nyumbani Kwa Baba wa Marehemu Ukonga Jijini Dsm. Aliyekuwa Katibu Wa CCM DMV Lovenes Mamuya na Wafiwa wengine wakisubiria kupokea Mwili wa Mpendwa wao Marehemu Zainab Buzohera unatogemea Kufika hii Leo Saa Nne Usiku kwa Muda wa hapa Tanzania
 
Naibu Katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba akitoa Pole kwa Mama mzazi wa Marehemu Zainab Buzohera alipokwenda kuhani Msiba Nyumbani Kwake Ukonga Banana hii Leo.
 
Mh:Mwigulu nchemba akitoa Mkono wa Pole kwa Bibi wa Marehemu Zainabu Buzohera.
 
Baba Mzazi wa Marehemu Zainabu Buzohera akibadilisha  mawazo na Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mh;Mwigulu Nchemba.Naibu katibu Mkuu alifahamiana na Marehemu Zainabu Buzohera wakati wa ziara ya Kichama kufungua Matawi Majimbo matano Nchini Marekani(Calfonia,Chicago,North Carolina,Mid West n,k) walishirikiana kwa Ukaribu sana Kuimarisha chama cha Mapinduzi kwa Upande wa Diaspora.
Mungu aipumzishe Roho Ya Marehemu Mahali Pema Peponi
AMINA

No comments:

Post a Comment