Mashahidi wanaripoti uporaji mkubwa wa
mali katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku kaimu rais mpya
akianza rasmi kazi yake. Mwandishi wa VOA Nick Long amabye yuko
mjini Bangui, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa maelfu ya watu walipora
mali katika eneo linalojulikana kama PK13 lenye wakazi wengi Waislam. Anasema majeshi ya Rwanda yaliwafukuza
waporaji, lakini uporaji ukaanza tena baada ya walinda amani hao wa
Rwanda kuondoka, kulinda sherehe za kuapishwa kwa kaimu rais mpya. Rais huyo mpya wa muda Catherine
Samba-Panza, ametoa mwito wa utulivu wiki hii kabla ya sherehe za
kuapishwa kwake, ambako kumefanyika katika majengo ya bunge leo Alhamis Chanzo, voaswahili.com
No comments:
Post a Comment