Pages

Friday, January 24, 2014

WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI WATAKA KUIMARISHWA KWA JUMUIYA HIYO.


eac_cbf2c.jpg
Bunge la Afrika Mashariki limeanza vikao vyake vya nne nchini Uganda na kuanza kwa kuzitolea mwito nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kutia bidii kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wanaijenga na kuiboresha jumuiya. Bunge la Afrika mashariki linafanya vikao vyake vya wiki moja nchini Uganda.
Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri amesema kuwa mazungumzo ya kujadili upya muundo wa muungano wa kisiasa wa Afrika Mashariki na mpango wa utekelezaji utazingatiwa mwezi wa April mwaka huu.
Miongoni mwa mambo ambayo muungano wa jumuiya ya Afrika mashariki unaweza kujivunia ni pamoja na kuweko na forodha moja ambayo ilitekelezwa tarehe moja mwezi huu. Pia, jumuiya iliweza kutia saini itifaki ya kuanzisha sarafu moja ya jumuiya.

Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na ambaye pia ni waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki nchini Kenya ametoa mwito kwa wabunge wazishinikize serikali zao zihakikishe kuhakikisha kuwa kutekelezwa kwa itifaki ya sarafu moja kunaanza tarehe moja mwezi wa Julai mwaka huu kama viongozi wa jumuiya walivyokubaliana walipokutana mara ya mwisho mwezi wa novemba mwaka uliopita.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Zziwa katika mkutano ya wanahabari alitangaza kwamba wataituma timu ya ukaguzi Sudan Kusini kukagua kama nchi hiyo iko tayari kujiungana jumuiya. Hii ni baada ya Sudan Kusini kuwasilisha rasmi ombi lao la kutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Timu hii itakuwa ikiangalia kama Sudan Kusini inatimiza misingi bora ya utawala kama vile demokrasia, utawala wa sheria, utunzaji wa haki za binadamu na haki za kijamii.
Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki kutoka Kenya Bi Kandie amewatakia heri raia wa Sudan Kusini na akasema kama majirani hawatawetekeleza haswa wakati huu wanapohitaji usaidizi.
Chanzo, voaswahili.com

No comments:

Post a Comment