Pages

Wednesday, January 8, 2014

RAMADHANI SINGANO AIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI YA MAPINDUZI CUP.




Mbali ya Azam FC timu nyingine zilizofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali jioni ya leo ni  URA na KCC zote za Uganda baada ya kupata ushindi dhidi ya KMKM NA Tusker ya Kenya katika michezo yao ya robo fainali.
URA imewafunga mabingwa wa Zanzibar  KMKM bao 1 kwa 0 ambapo bao hilo pekee na la ushindi limefungwa na  Owen Kasule dakika ya 42 Uwanja wa Gombani, Pemba wakati KCC imeitoa kwa mikwaju ya penalti 4 kwa 3 dhidi ya Tusker kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar
Kipa wa KCC, Omar Magoola alipangua penalti mbili ya Ismail Dunga na Luke Ochieng, wakati za Clifford Alwanga, Brian Osumba na kipa mwenzake Samuel Odhiambo zikitinga nyavuni.

TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE)


Waliofunga penalti za KCC ni Tony Odur, Habib Kavuma, Stephen Bengo na kipa Omar Magoola na kwa matokeo hayo, KCC itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza kesho kutwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar Saa 10:00 jioni.  



Robo Fainali ya mwisho imemalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan baada ya wekundu wa Msimbazi Simba SC kuifunga Chuoni mabao 2-0,mabao hayo yamefungwa na Ramadhan Singano,kwa ushindi huo Simba itacheza  na URA katika Nusu Fainali ya pili kesho kutwa Saa 2:00 Usiku.

No comments:

Post a Comment