Pages

Wednesday, January 8, 2014

SMART TOOTHBRUSH: MSWAKI UNAOMPA TAARIFA MTUMIAJI KUPITIA SMARTPHONE WAKATI WA KUSAFISHA KINYWA


Wale mnaopenda vitu smart, kama smartphone, smartwatch, smarthome, sasa mnaletewa smart toothbrush, mswaki ambao unauwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji kupitia simu ya mkononi.
The Kolibree toothbrush imetengenezewa kifaa maalum (sensor), na inatumia app kumuonesha mtumiaji kila sehemu mswaki huo unapopita kinywani na kumshtua endapo ataruka sehemu.
Pia mswaki huo unamjulisha mtumiaji kama amesafisha kinywa kwa muda wa kutosha na kama amesafisha sehemu zote muhimu za kinywa.
Taarifa zote kutoka kwenye mswaki huo zitaonekana katika smartphone ya Android na iOS ya mtumiaji kwa kupitia bluetooth.
Smart toothbrush zitaanza kuuzwa baada ya April mwakaa huu kwa $100.

No comments:

Post a Comment