Pages

Tuesday, January 7, 2014

TAARIFA YA KUAHIRISHWA KWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA YA LEO JUMANNE JANUARI 07, 2014 HADI KESHOKUTWA ALHAMIS JANUARI 09, 2014!


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Jumanne Januari 07, 2014 saa 3 usiku kwenda bara imeahirishwa hadi keshokuwa siku ya Alhamis Januari 09, 2014, saa 3 usiku.


TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI ZA KILA SIKU,(USIPITWEEEEEEEE) 
Taarifa imefafanua kuwa dharura hiyo imetokana na ajali ya treni ya mizigo iliyotokea juzi saa 2 usiku kati ya Stesheni za Luiche na Kigoma na kusababisha treni ya abiria kutoka Kigoma kushindwa kuondoka kuja Dar.
Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio tokea juzi usiku na taarifa za uhakika zinaeleza kuwa zoezi la kuondoa mabehewa matatu ya treni ya mizigo yalioanguka na kukarabati njia ya treni litakamilika leo Jumanne Januari 07, 2014.
Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji
Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Januari 07, 2014

No comments:

Post a Comment