Pages

Thursday, January 9, 2014

TAARIFA YA MSIBA:ANNA JOHN MBONDE AMEFARIKI DUNIA


Familia ya Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Muleba ,Iringa  na Njombe ,ndugu John Pantaleon Mbonde wa Ilala Sharif Shamba Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha mtoto wake mpendwa Anna Mbonde. Marehemu alifikwa na mauti tarehe 5/1/2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. Marehemu alisumbuliwa na ugonjwa wa seli mundu (yaani sickle cell disease) pia alikuwa na matatizo ya figo kwa muda wa mwaka mmoja uliopita. Mazishi yalifanyika juzi 7/1/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni.Familia inatoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza katika shughuli nzima ya mazishi.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMINA

No comments:

Post a Comment