Pages

Wednesday, January 8, 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA::UNYAMA KIKONGWE ACHINJWA KAMA KUKU HUKO KAHAMA,UCHAWI WAHUSISHWA



Mwanamke mmoja Alifahamika kwa jina la Milembe Jengamalulu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 50-55, mkazi wa Ulowa no 4 wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umri wa miaka 50-55, amefariki dunia baada ya kuchinjwa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikani.
MWILI wa Marehemu Milembe Jengamalulu ukiwa eneo la tukioKwa mujibu wa majirani tukio hilo limetokea katika mkesha wa mwaka mpya majira ya saa moja usiku, nyumbani kwake maeneo ya Ulowa no 4 ambapo kikongwe huyo alikuwa anaishi na mtoto wake wa kiume.
Wameeleza kuwa Wakati tukio hilo likitokea, mtoto wake wa kiume ambaye hakutajwa jina lake (miaka 34-40) alikuwa ameenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya akiwa na mkewe maeneo ya Ulowa no 5, na wote walirudi nyumbani majira ya saa 10 na usiku ndipo walikuta mwili wa marehemu Milembe Jengamalulu.
Baada ya kuukuta mwili huo ukiwa nje ya nyumba huku ukiwa umetapakaa damu nyingi, huku ukionesha kuwa amechijwa kwa kutumia panga na shoka, walitoa taarifa kwa majirani ambao walisaidia kutoa taarifa kwa uongozi. 

No comments:

Post a Comment