Mgomo mkubwa zaidi wa
wafanyakazi wa machimbo ya madini ya Platinum nchini Afrika Kusini,
utaanza siku ya Alhamisi, kulalamikia mishahara duni.
Mgomo huo utasitisha uchimbaji wa madini hayo
katika migodi ya kampuni tatu mikubwa zaidi duniani kwa uzalishaji wa
madini ya Platinum.Huu ni mgomo mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika secta ya uchimbaji wa madini ya Platinum tangu mkasa wa mwaka juzi wa Marikana ambapo wachimba migodi wapatao 34 walipigwa risasi na polisi walipokuwa wakiandamana kuendeleza mgomo wao , uliotajwa na serikali kuwa haramu.
Mgomo halali
Safari hii gomo huu wa kudai nyongeza ya mishahara unaongozwa na AMCU chama cheye msimamo mkali cha kutetea wafanyaki wa migodini na mafundi katika sekta ya ujenzi.Tofauti na mgomo wa Marikana, mgomo huu wa sasa ni halali kisheria.
Kampuni zote tatu za Anglo American, Impala na Lonmin Platinum zimethibitisha kupokea notisi za mgomo.
Hata hivyo wanadai hawawezi kumudu kulipa nyongeza hiyo inayodaiwa kwa sababu ya gharama za uzalishaji ni kubwa na mauzo ni haba.
Afrika Kusini ndio nchi inayozalisha madini ya Platinum kwa wingi zaidi huku asilimia 80% ya madini hayo yakiwa bado hayajachimbwa.
No comments:
Post a Comment