Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 29, 2014

WAKAZI WA DODOMA WAMETAKIWA KUJIPANGA ILI KUHAKIKISHA WANAPATA KATIBA MPYA YENYE HAKI NA USAWA KWA TAIFA LA TANZANIA.


Akizungumza  na wanachi wa Manispaa ya Dodoma  katika mkutano wao wa mwisho  uliofanyika  hapo jana katika viwanja vya barafu Mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo   Mh Tundu lisu  amewataka wananchi  kufahamu umuhimu wa katiba  mpya ili kuepukana  na  migogoro.
Aidha  Tundu Lisu  amewaomba wananchi kujitokeza   kujiandikisha  katika daftari la wapiga kura  katika kipindi hiki  cha  uchaguzi wa  Madiwani na uraisi ili kupata haki ya kumchagua  kiongozi  wanae mtaka.
Nae Mwenyekiti wa  baraza la vijana  Chadema Taifa  BAVICHA  Mh  John Heche  ameongezea kuwa hawata  wavumulia viongozi wanaovuruga chama bali  watawachukulia  hatua mara  moja na kuwandoa  ndani ya chama hicho .
Wakizungumza katika mkutano huo baazi ya wakazi wa manispaa Dodoma  wamesema wameupokea kwa furaha mkutano huo kwani wanahitaji  mabadiliko katika taifa la Tanzania.NA DODOMA FM

No comments:

Post a Comment