bendera
ikionekana imechanika kwenye ufukwe wa Scituate Massachusetts baada ya
tufani ya theluji iliyoanguka siku ya alhamisi Jan 2, 2014 na
kusababisha vifo vya watu 9 mji wa Boston imeanguka theluji ipatayo futi
2 na kusababisha kufunga barabara kuu inayounganisha Pennsylvani, New
York na Boston, viwanja vya ndege, Mssachusetts, New York vilisitisha
safari za ndege mpaka hapo theluji itakapokwanguliwa na hali kuwa salama
kwa ndege kuruka. Meya wa New York ilibidi atangaze hali ya dharura
(State of Emergency) kwa wakazi wa jiji hilo lisilolala. Picha na
Michael Dwyer
mpiga
picha akipata ukodak moment kwa sananmu iliyotengenezwa kwa theluji
karibu na Capitol Hill mjini Washington, DC. ambapo theluji ilianguka
ipatayo inchi 3 mpaka 5 kwa maeneo mengine ya Virginia na Maryland.
picha na Evan Vucc
Daraja la
RFK New York lilivyokua likionekana siku ya Ijumaa Jan 3, 2014 baada ya
theluji kuanguka siku ya alhamis jioni na kusababisha shule na ofisi za
serikali kufungwa. Picha na John Minchillo
Watembea
kwa miguu wakivuka barabara siku ya alhamisi kwenye jiji lisilolala la
New York wakati theluji ilipokua ikidondoka. picha na John Minchillo
Maeneo ya Time Square yalivyoakua yakionekana wakati theluji ilivyokua ikianguka
picha na John Minchillo
No comments:
Post a Comment