Balozi
wa mpya wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Aziz Ponery Mlima leo asubuhi
ametembelea Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na kukutana na viongozi wa
Ofisi hiyo.Pamoja
na mambo mengine waliozungumza, viongozi hao waliongelea diplomasia ya
uchumi, maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Malaysia kwa ujumla.
Dkt.
Mlima aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete, mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana kuwa Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kuala Lumpur, Malaysia, ambayo
imekuwa ikiisadia Tanzania katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo,
ikiwemo utaratibu mpya wa kusamimia miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment