Lionel
Messi amefunga mara mbili wakati klabu yake ya Barcelona ikijiandaa na
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jumanne ijayo dhidi ya Manchester City
kwa kuichapa bila huruma Rayo Vallecano mabao 6-0 na kujikita kileleni
mwa msimamo wa La Liga.
Mlinzi wa kushoto Adriano alifunga bao la ufunguzi kabla Messi hajapiga bao la pili.
Mabao mengine yamefungwa na Alexis Sanchez, Pedro, Messi na Neymar.
Katika mchezo mwingine wa La Liga, Atletico Madrid imeichapa Real Valladolid mabao 3-0. Mabao ya washindi yakifungwa na kiungo Raul Garcia, Diego Costa na mlinzi Diego Godin.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
No comments:
Post a Comment