Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 16, 2014

Barcelona waitandika Rayo Vallecano Goli 6 Bila

Lionel Messi amefunga mara mbili wakati klabu yake ya Barcelona ikijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jumanne ijayo dhidi ya Manchester City kwa kuichapa bila huruma Rayo Vallecano mabao 6-0 na kujikita kileleni mwa msimamo wa La Liga.
Mlinzi wa kushoto Adriano alifunga bao la ufunguzi kabla Messi hajapiga bao la pili.


Mabao mengine yamefungwa na Alexis Sanchez, Pedro, Messi na Neymar.
Katika mchezo mwingine wa La Liga, Atletico Madrid imeichapa Real Valladolid mabao 3-0. Mabao ya washindi yakifungwa na kiungo Raul Garcia, Diego Costa na mlinzi Diego Godin.
Nayo Levante imeichapa Almeria 1-0 na Villarreal imekubali kipigo cha 2-0 kutoka kwa Celta de Vigo
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

No comments:

Post a Comment