Wafuasi
wa CCM Iringa wakimpongeza kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan
Mtenga kwa kufanikisha chama hicho kushinda uchaguzi mdogo kata ya
Nduli.
Wafuasi
wa CCM kata ya Nduli wakiwa wamemnyanyua juu juu aliyekuwa mgombea
udiwani kata ya Nduli Bw Mtove baada ya matokeo kumpa ushindi wa
kishindo leo
...........................
CHAMA
cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefanikiwa kutetea kata
zake zote tatu ambazo leo wananchi wameshiriki kupiga kura
kuwachagua madiwani kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani
wake kufariki dunia.
Wafuasia
wa CCM walimpongeza aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja
na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga na kudai kuwa
kazi yake inaonesha wazi safari yake ya kulitwaa jimbo la Iringa
mjini.
Matokeo
katika vituo vyote tisa ambavyo wananchi wa Nduli walipata
kuvitumia kupiga kura ,kituo cha Mawasiliano CCM
(57),Chadema(28),Zahanati CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli
CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata
CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni CCM(138
,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina CCM (156 ) Chadema
(31)
Katika
Matokeo hayo ambayo hadi sasa majira ya saa 12.50 bado msimamizi wa
uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku hadema wakifuatia
kwa kura 487,Mbali ya matokeo hayo ya kata ya Nduli pia CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za wilaya ya Kilolo.
Katika
kata ya Njombe mjini mgombea wa Chadema amembwaga mgombea wa CCM
ambapo matokeo yanaonyesha mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja
pekee kwa tofauti ya kura 2 huku katika vituo vyote Chadema
ikiibuka kidedea.NA MICHUZI JR
No comments:
Post a Comment