Pages

Sunday, February 9, 2014

CCM WASHINDA KATA ZOTE TATU MKOA WA IRINGA, CHADEMA YASHINDA NJOMBE MJINI



 Wafuasi wa CCM Iringa  wakimpongeza kaimu katibu  wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha  chama  hicho kushinda  uchaguzi mdogo kata ya  Nduli.
Wafuasi wa CCM kata ya Nduli  wakiwa  wamemnyanyua  juu  juu  aliyekuwa mgombea  udiwani kata ya Nduli Bw Mtove  baada ya  matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo 
...........................
CHAMA  cha  mapinduzi (CCM)  mkoa  wa  Iringa  kimefanikiwa  kutetea kata  zake  zote tatu ambazo  leo   wananchi  wameshiriki  kupiga kura  kuwachagua madiwani  kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki  dunia.
Wafuasia  wa  CCM  walimpongeza  aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na  kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Hassan Mtenga na kudai kuwa  kazi  yake  inaonesha  wazi  safari yake ya  kulitwaa jimbo la Iringa mjini.
Matokeo katika vituo vyote  tisa  ambavyo  wananchi  wa Nduli  walipata  kuvitumia kupiga kura  ,kituo cha Mawasiliano  CCM (57),Chadema(28),Zahanati  CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli  CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni   CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina  CCM (156 ) Chadema (31)

Katika  Matokeo hayo ambayo hadi sasa  majira ya saa 12.50  bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku  hadema  wakifuatia kwa kura 487,Mbali ya  matokeo  hayo ya kata ya  Nduli pia  CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za  wilaya ya  Kilolo.

Katika kata ya  Njombe mjini mgombea  wa  Chadema amembwaga mgombea wa CCM ambapo  matokeo yanaonyesha  mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja pekee   kwa tofauti ya  kura  2  huku  katika vituo vyote  Chadema ikiibuka kidedea.NA MICHUZI JR

No comments:

Post a Comment