Pages

Sunday, February 9, 2014

DR MWAKYEMBE AMNADI MGOMBEA UDIWANI WA NJOMBE MJINI AWAONYA CCM KUACHA KUNUNULIKA

 mgombe  udiwani  kata  ya Njombe mjini BW.MLYUKA  akiomba  kura  leo


 Waziri Dr Mwakyembe  akifunga kampeni  wa  udiwani kata ya  Njombe mjini  leo
 Bw Mlyuka  akiomba  kura  leo 
Mgombea udiwani kata ya  Njombe mjini Bw Mlyuka  akiomba kura  leo katika ukumbi wa Turbo Njombe
...................................................................................................................................
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aonya  wana CCM kuachana kununuliwa kwa pesa  ndogo ndogo badala ya kujengewa  misingi ya maendeleo.
Dr Mwakyembe alitoa kauli  hiyo leo wakati akimnadi  mgombea udiwani wa  CCM kata ya  Njombe mjini Menardy Mlyuka  na kuwataka wana CCM kuachana na tabia ya  kujirahisi kwa wana CCM  wasio na nia njema na moja na ushirikiano uliopo katika chama hicho.
Hata  hivyo  alisema  kuwa chama  hicho  kitaendelea  kushinda katika chaguzi mbali mbali  kutokana na umoja  uliopo na CCM ina mengi ya  kuwaonyesha  watanzania  ukilinganisha na vyama vya upinzani.
Pia  Dr  Mwakyembe  ametoa  muda wa miezi  mitatu  kuanzia sasa  kuona stendi  kuu ya mkoa  wa Njombe  inaboreshwa vilivyo vinginevyo mkurugenzi  na mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe  mji  wanapaswa kujitathimini kama  wanatosha ama wanapaswa kuachia nafasi.
Alisema  kuwa  hajapendezwa na ubovu wa stendi  hiyo ya Njombe na hivyo kuwataka  viongozi na  wilaya  hiyo kujipanga kuboresha  stendi   hiyo badala ya  kuendelea  kuiacha kama ilivyo.
Pia  alisema kuwa  chama  cha  CCM kitaendelea  kushika dola kutokana na kuendelea  kuwatumikia  watanzania kwa  vitendo na siku  zote  kwanda  kwa  wananchi na hoja zinazoeleweka tofauti na  vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa  vikija  na hoja za  juu juu.
CCM itaendelea  kutawala  daima  na  kuendelea  kushinda chaguzi mbali mbali kutokana na mambo makubwa ambayo kimeyafanya .
Dr  Mwakyembe  alisemakuwa kwa jupande wa  Njombe  wizara yake  imekusudia  kujenga  kiwanja  cha Kisasa  katika mji huo kupitia pesa  za wahisani  wa  benk ya  dunia.

No comments:

Post a Comment