...................................................................................................................................
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aonya wana CCM kuachana kununuliwa kwa pesa ndogo ndogo badala ya kujengewa misingi ya maendeleo.
Dr
Mwakyembe alitoa kauli hiyo leo wakati akimnadi mgombea udiwani
wa CCM kata ya Njombe mjini Menardy Mlyuka na kuwataka wana CCM
kuachana na tabia ya kujirahisi kwa wana CCM wasio na nia njema na
moja na ushirikiano uliopo katika chama hicho.
Hata hivyo alisema kuwa
chama hicho kitaendelea kushinda katika chaguzi mbali
mbali kutokana na umoja uliopo na CCM ina mengi
ya kuwaonyesha watanzania ukilinganisha na vyama vya upinzani.
Pia Dr Mwakyembe ametoa muda
wa miezi mitatu kuanzia sasa kuona stendi kuu ya mkoa wa
Njombe inaboreshwa vilivyo vinginevyo mkurugenzi na mwenyekiti wa
Halmashauri ya Njombe mji wanapaswa kujitathimini kama wanatosha
ama wanapaswa kuachia nafasi.
Alisema kuwa hajapendezwa
na ubovu wa stendi hiyo ya Njombe na hivyo kuwataka viongozi
na wilaya hiyo kujipanga kuboresha stendi hiyo badala
ya kuendelea kuiacha kama ilivyo.
Pia alisema
kuwa chama cha CCM kitaendelea kushika dola kutokana na
kuendelea kuwatumikia watanzania kwa vitendo na
siku zote kwanda kwa wananchi na hoja zinazoeleweka tofauti
na vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikija na hoja za juu juu.
CCM itaendelea kutawala daima na kuendelea kushinda chaguzi mbali mbali kutokana na mambo makubwa ambayo kimeyafanya .
Dr Mwakyembe alisemakuwa
kwa jupande wa Njombe wizara yake imekusudia kujenga kiwanja cha
Kisasa katika mji huo kupitia pesa za wahisani wa benk ya dunia.
No comments:
Post a Comment