Pages

Thursday, February 20, 2014

Hii ndiyo timu ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge la Katiba

 
Dodoma. Suala la posho limezidi kuwa kaa la moto katika vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma leo, hali iliyomlazimu mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho ateue timu maalum ya watu 6 kutazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo.

Timu hiyo inatarajiwa kuyachunguza kwa undani mahitaji ya wajumbe wa Katiba, kisha kuisaidia serikali kutafuta jinsi ya kuongeza posho hizo.
Wajumbe wa timu ya posho ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Wengine ni mjumbe wa asasi zisizo za kiserikali Paul Kimiti, Mbunge wa Peramiho Jenister Mhagama (CCM) na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Asha Bakari na Mohamed Aboud Mohamed.

No comments:

Post a Comment