Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM), Mchungaji Lackson Mwanjale
Mbunge wa
Mbeya Vijijini (CCM), Mchungaji Lackson Mwanjale na Katibu wa Uchumi wa
Wilaya, Shadrack Mwanjuguja walijeruhiwa kwa mapamga katika Kata ya
Santilya, iliyopo Halmashauri ya Mbeya Vijijini.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya, Maganga Sengerema, alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo jana saa 4:00 asubuhi. Hata hivyo, hakufafanua.
“Tukio hilo limetokea kweli. Mbunge wetu amepigwa. Lakini utaratibu
wangu ni kwamba, siwezi kutoa maelezo zaidi ya tukio kwa kuzungumza na
mtu kwenye simu. Kama unataka njoo hapa ofisini kwangu,” alisema.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa, ambazo NIPASHE imezipata kutoka
eneo la tukio na kuthibitisha na vyombo vya ulinzi na usalama, mbunge
huyo alipigwa na watu wasiojulikana akiwa katika kituo cha kupigia kura
cha Shicongo.
Taarifa zinaeleza kuwa mbunge huyo amejeruhiwa kichwani na kushonwa nyuzi kadhaa katika kituo cha afya cha Ilembo.
MKASA ULIVYOTOKEA
Wakati wananchi wakiendelea kupiga kura katika kituo hicho, walifika vijana kadhaa wanaodai kuwa ni wafuasi wa Chadema.
Vijana wa CCM walianza kuwahoji wamekwenda kufanya nini katika kituo hicho.
Vijana wa Chadema walijibu kuwa wao ni mawakala. Majibu hayo hayakuwaridhisha vijana wa CCM.
Habari zinasema kuwa vijana wa CCM walipiga simu polisi, ambao
walifika katika kituo hicho na kuwaondoa vijana wa Chadema. Muda mfupi
baada ya kuondolewa vijana hao, Mchungaji Mwanjale alifika katika kituo
hicho akiwa na Katibu wa Uchumi wa Wilaya na ndipo kukazuka vurugu
akaanza kushambuliwa kwa mapanga.
Katika vurugu hizo, matairi ya gari la mbunge huyo lenye namba za
usajili T 222 AKG yaliondolewa upepo. Baadaye polisi walifika eneo la
tukio na kumuokoa mbunge huyo.
Kufuatia vurugu hizo watu saba wametiwa mbaroni. Mchungaji Mwanjale
aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa alivamiwa na vijana waliokuwa na
pikipiki ambao walimtuhumu kuhusika na kushambiliwa kwa mwezao ambaye
hata hivyo hawakumtaja.
Alisema kuwa alipokana kuhusika na mashambulizi hayo, vijana hao
walikuwa na silaha mbalimbali za jadi, walimshambuliwa na kumuuza
kichwani.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment