Gazeti
hilo limeendelea kuandika kuwa wiki hii Rais Jakaya Kikwete, atakutana
na Prince of Wales, Duke of Cambridge, Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron na Rais mambo ya nje wa nchi hiyo, William Hague kwenye mkutano
wa viongozi wa nchi 50 huku Tanzania ikiwa na sifa mbaya kwa mauaji ya
Tembo.
Mkutano huo ni mahsusi kwaajili ya kuokoa viumbe hao wanaohatarishwa kupotea kutokana na kushamiri kwa mauaji.
Mkutano
huo wa Alhamis hii utajaribu kufikia muafaka kuhusiana na muitikio wa
kidunia dhidi ya biashara haramu ya pembe za ndovu yenye thamani ya
paundi bilioni 6 kwa mwaka na ambayo hudhamini makundi ya kigaidi.
Theluthi
ya pembe zote za ndovu zinazokamatwa barani Asia hupitia Tanzania na
kila siku tembo 30 huuliwa ambao ni sawa na tembo 11,000 kila mwaka.
“Tanzania
is effectively a one-party state with a pervasive intelligence
apparatus, and nobody seriously contends that this slaughter is
happening without high-level complicity. Yet not a single kingpin has
been charged and convicted. MPs, senior officials and businessmen are
named in parliament and the media, but investigations fizzle out and
little happens,” Daily Mail wameandika.
Katika gazeti la leo la MWANANCHI la nchini Tanzania limeandika habari hii kwa kina kwa ufupi linasema ‘Kwa
jumla Tanzania inatawaliwa na chama kimoja ikiwa chini ya chombo kimoja
cha intelijensia, hakuna mtu anayepinga kuwa hayo yanafanyika bila
kuhusisha ngazi za juu. Lakini hakuna hata kigogo mmoja aliyekamatwa na
kushtakiwa.” Inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment