Pages

Friday, February 21, 2014

JAJI WEREMA AWATAKA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUTOCHEZEA TUNU ZA TAIFA NA MUUNGANO

habariMwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick  Werema akizungumza na wajumbe wenzake  wa bunge maalum la katiba katikaka viwanja vya bunge mjini Dodoma kushoto ni Dr. Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
NA  MAGRETH KINABO –MAELEZO
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji  Fredrick  Werema amewataka wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba  kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya  kwa jinsi wanavyotaka,lakini wasiondoe misingi mikuu ya kitaifa(tunu za taifa) na maadili ya jamii ya kuhifadhi na kudumisha mambo ya misingi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Werema wakati akitoa semina kwa wajumbe hao leo mjini Dodoma kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Bunge la Katiba Sura ya 83 toleo la mwaka 2014.
“ Ifanyieni  Rasimu ya Katiba Mpya mnavyotaka, lakini , yana mipaka yake.  Fanyeni mnachotaka ila msifanye jambo lolote litakaloondoa uwepo wa Jamhuri ya Muungano ,” alisema  Jaji Werema.


 Jaji Werema aliyataja mambo hayo ambayo yapo katika  kifungu cha 9(2) katika sheria hiyo ambayo ni  kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano, uwepo wa Serikali ,Bunge na Mahakama, mfumo wa kiutawala wa kijamhuri, uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, umoja wa kitaifa,amani na utulivu, uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote wenye sifa ya kupiga kura.
Mambo mengine ni , ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu, utu,usawa mbele ya sheria na mwenendo wa sheria, uwepo wa Jamhuri ya Muungano isiyofungamana na dini yoyote na inayoheshimu uhuru wa kuabudu .
Alisema Jaji  Werema huku aelezea kuwa itakuwa si sahihi misingi hiyo , ambayo tume imeongozwa  nayo  itofautiane na Bunge Maalum la Katiba.
Jaji Werema  alitoa ufafanuzi kuhusu kifungu cha 25(1) kufuatia baadhi ya wajumbe kutaka ufafanuzi ambao ni Tundu Lissu  kuhoji kuwa hakina uhusiano na bunge hilo na Zitto Kabwe kutaka ufafanuzi  na kudai kuwa kumekuwepo na vikundi vya vyama vina rasimu mbadala je Bunge hilo lina mamlaka ya kuweka pembeni maoni ya wananchi.
  Aliongeza kuwa Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na masharti yaokanayokama Bunge Maalum litakavyoona inafaa.
 Jaji Werema alisema kifungu hicho(20) Mamlaka ya Bunge Maalum ya kupitisha masharti ya Katiba inayopendekezwa baada ya Rasimu ya Katiba kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Tume na Kupitishwa na Bunge Maalum.
Hivyo wajumbe hao ni wawakilishi wa wananchi watafanya kazi ya kuiboresha na baade itarudi kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni.
Kuhusu suala kuwa mitaani kuna rasimu katiba mbadala alisema suala hilo ni upotoshaji.
Aidha  Jaji Werema aliwataka wajumbe hao kuwasilisha hoja kwa stahaa na kupeana uhuru wa kutoa maoni.

No comments:

Post a Comment