Pages

Friday, February 21, 2014

JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA LAWASHIKILIA WATU SABA.


JESHI la polisi mkoani Iringa linawashikilia watu saba kwa makosa tofauti tofauti likiwemo la mkazi wa Makongati Tarafa ya Mololo aitwaye Mario Kibodya (30) kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili jina limehifadhiwa (8) na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
 
Akizungumza  ofisini kwake Kaimu kamanda wa polisi Mrakibu mwandamizi Peter Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 20 februari majira ya saa 9 kamili mchana.
 
Wakati huohuo mkulima aliyefahamika kwa jina la Junus Mkovano (35) mkazi wa Mgama tarafa ya Kiponzero anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumbaka mkulima mwenzake aitwaye Lucy Bahary (41).
 
Kaimu Kakamba alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 20 februari majira ya saa 1 kamili asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo alimvamia mwanamke huyo akiwa shambani na kumfanyia kitendo hicho na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.
 
Mbali na matukio hayo mawili ya ubakaji Kaimu Kakamba alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi  mkoani Iringa kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi misokoto 123.
 
Kamanda Kakamba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watuhumiwa hao ni Joseph Lihundi, Justine Mwelungo, Benedict Nzuki, Baraka Malinga pamoja na Nathani Simon ambao walikamatwa na askari wakiwa doria maeneo ya Makorongoni.
 
 
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIO DAIMA.COM, IRINGA

No comments:

Post a Comment